Raia 9 wa Eritrea na wawili Ethiopia wapigwa faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
February 24, 2025
By Mark Dida,
Mwanafunzi mmoja anadaiwa kuuliwa na polisi kwa kupigwa risasi majira ya saa mbili jioni, hapo jana katika mjii wa Mandera.
Kulingana na familia, Zakariah Mohamed alipigwa risasi alipokuwa akitoka masomo ya ziada huku wakiandamana na walimu wake.
Mvulana huyo alikibizwa katika hospitali ya rufaa mjini Mandera ila akiripotiwa kufariki muda mchache baada ya kufikishwa hospitalini.
Askari wanaodaiwa kutenda kitendo hicho cha unyama wamenyanganywa silaha huku uchuguzi ukiaza rasmi kubaini kini cha kisa hicho.
Aidha wakaazi wa eneo hilo wanataka serikali kuchukulia hatua kwa maafisa wa polisi wanaodaiwa kutenda kitendo hicho