Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Machuki Denson.
Kaunti ya Baringo imekuwa ya kwanza kuupinga na kuangusha mswada wa BBI.
Hii ni baada ya patashika nguo kuchanika ndani ya bunge hilo jana. MaMCA watanao pekee ndio walihesabiwa kupioga kura ya kuidhinisha mswada huo wakati madiwani wenzao 30 wakipiga kura ya kuupinga.
Madiwani watano walisusia zoezi hilo.
Vitoza machozi vilirushwa ndani ya bunge hili wakati madiwani walionekana kukabiliana wakati wa kujadili na kupiga kura. Hii ilikuwa baada ya madiwani wa KANU kukabiliana na wale wa Jubilee ndani ya bunge hilo. Aidha hiyo jana Bunge la Kaunti ya Homabay lilikuwa la tatu kupitisha kwa kauli moja, mswada huo.
Mswada huo wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano BBI,umewasilishwa katika bunge hilo hii leo na kupitishwa na wanachama wa bunge hilo.
Kaunti za Siaya na Kisumu ndizo zilizokuwa za kwanza kupitisha mswada huo ambao uliwasilishwa kwenye mabunge yote 47 ya kaunti humu nchini na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ili ujadiliwe.
Awali, Bunge la Kaunti ya Homabay lilikuwa limetoa nafasi kwa umma kutoa maoni yao kuhusu mswada huo kufikia jana Jumatano.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya Kiongozi wa ODM Raila Odinga kukutana na mamia ya viongozi na wajumbe kutoka kaunti hiyo kwenye kikao cha uhamasisho kuhusu BBI.
Mswada huo unahitaji kuidhinishwa na angalau mabunge 24 ya kaunti ili uweze kuelekea kwenye hatua ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa na la Seneti.
Mabunge ya Kaunti yana hadi tarehe 26 mwezi Aprili kufanya maamuzi kuhusu mswada huo.