Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Isaac Waihenya,
Jamii za Garre na Murule ambazo zimekuwa zikizozana Katika kaunti ya Mandela Zimetoa maazimio yao kwa tume ya uiano na utengamano Nchini NCIC kama njia mojawapo ya kumaliza uhasama Katika eneo hilo.
Maazimio hayo yaliyosomwa mbele ya wazee wa jamii hizo mbili pamoja na viongozi wa kaunti na wa serekali yamesema kuwa jamii inayotuhumiwa kuwa na makosa kunapotokea mgogoro inafaa kulipa faini ya ngamia 350 au pesa sawa na idadi hiyo.
Aidha jamii hizo zimekubaliana kuwa mali iliyoibiwa Kutoka pande zote mbili za jamii hizo irejeshwa kwa muda wa wiki mbili huku swala la mipaka na ambalo limetajwa kuwa chanzo cha mzozo likiangaziwa.
Aidha mwenyekiti wa tume ya Uiano Daktari Samuel Kobia amesifia hatua hiyo na kuzitaka jamii zingine zinazozana Katika maeneo ya kasakazini mwa nchi kuiga mfano huo.