Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit yalaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha katika eneo la Dololo,North Horr.
January 23, 2025
regional updates and news
WANAFUNZI 19 kati ya 20 kutoka shule ya upili ya Ngurnit iliyo eneobunge la Laisamis watajiunga na vyuo vikuu kutokana na wao kujizolea alama ya C+ kwenda juu. Kulingana na matokeo ya shule hiyo ni kuwa wanafunzi 8 walipata alama ya B (plain), sita walipata B-, watano wakipata C+ na[Read More…]
Wakaazi wa eneo la Karare,eneo bunge la Saku, kaunti ya Marsabit wamenufaika na msaada wa chakula na vifaa vingine vya matumizi kutoka kwa katibu wa maeneo kame na maendeleo ya mikoa nchini Kello Harsama. Msaada huo unajumuisha vyakula, blanketi pamoja na taulo za kutumiwa na wanawake na wasichana wakati wa[Read More…]
Viongozi wa vijana viungani mwa mji wa Laisamis kaunti ya Marsabit wameonya wazee walio na hulka ya kuuza ardhi ya familia ovyo ovyo kwa bei ya kutupa. Vijana hao kutoka eneo la Manyatta Secondary wakiongozwa na kiongozi wao Mwl. Lito Herkena ameambia shajara kuwa kuna baadhi ya wazee katika eneo[Read More…]
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuhakikisha kwamba wanao wanaripoti shuleni kwa muhula wa kwanza wa mwaka wa 2025. Kwa mijibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit Mukanzi Leakey ni kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu huku akionya kuwa idara hiyo haitawasaza wazazi watakaokosa kuwapeleka wanao shuleni[Read More…]
Idara ya utabiri wa hali ya hewa hapa Marsabit imesema kuwa hali ya kiangazi itazidi kushuhudiwa mwezi huu Mkurugenzi wa utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Marsabit Abdi Dokata amesema kuwa kiangazi itaendelea kwa sasa hadi wakati utabiri utakapobadilika. Ameshauri wananchi wa Marsabit kuepuka kutembea kwenye jua na kunywa maji mengi msimu huu[Read More…]
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi ya Bakaka iliyoko eneo la Hurii hills eneo bunge la North horr Ibrae Sharamo amelalamikia kile amekitaja kwamba ni ukosefu wa madarasa ya gredi ya tisa. Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Sharamo ametaja kwamba hadi kufikia sasa wanafunzi 17 wa[Read More…]
Baadhi ya Magavana, yule wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir na Julius Malombe wa Kitui wamepinga mfumo mpya wa ugavi wa fedha kwa serikali za kaunti unaopendekezwa na Tume ya Ugavi wa Mapato kwa kaunti, CRA. Mfumo huo mpya uliopendekezwa na CRA unapendekeza mgao wa shilingi bilioni 417 kwa Kila kaunti huku kaunti[Read More…]
Usalama umeimarika kwa kiwango kikubwa katika kaunti ndogo ya Loiyangalani hii ni baada ya vitengo vya usalama kuendesha operesheni ya kutoa hamasa kwa wakazi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa OCPD wa eneo hilo Nicholas Mutua ni kuwa kupitia ushirikiano wa maafisa wa usalama pamoja na wakazi katika eneo hilo[Read More…]
Huku shule zikifunguliwa kwa muhula wa kwanza wa mwaka 2025 leo jumatatu, wazazi wameonywa dhidi ya kutowapeleka wanao shuleni. Ni onyo ambalo limetolewa na Chifu wa eneo la Laisamis Agostino Supeer akisema kuwa wazazi watakao kiuka haki za watoto kupata elimu watawajibishwa kisheria. Chifu Supeer aliyezungumza na meza ya habari ya[Read More…]
Serekali inapania kujenga shule katika sehemu mbazo hazina shule, kaunti ya Marsabit ili kuzuia wanafunzi kusafiri mbali kusaka elimu. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa idara ya elimu jimboni chini ya uongozi wake imependekeza kwa wizara ya elimu hoja ya kujengwa kwa[Read More…]