Local Bulletins

Wakaazi wa eneo la Arge,Marsabit walalamikia kile wamekitaja kuwa mnyama anayetisha…

Na Isaac Waihenya,

Wakaazi wa eneo la Arge, lokesheni ya South Horr, wadi ya Kargi, kaunti ndogo ya Loiyangalani, kaunti ya Marsabit wanahofia maisha yao baada ya kuona kiumbe kisichojulikana kikirandaranda katika vijiji cha Arge karibu na mradi wa Lake Turkana Wind Power.

Kulingana na naibu chifu wa eneo la South Horr, Jonathan Ogom, mnyama huyo aliripotiwa mara ya kwanza na wafugaji ambao waliona nyayo zisizo za kawaida.

Baadaye hofu yao ilithibitishwa baada ya wakaazi hao kushuhudia kiumbe hicho mmoja kwa moja.

Maelezo ya mnyama ni kwamba; atembea lakini sio wima kabisa kama binadamu, na ana kimo kibwa cha mwili uliojaa nywele kama Sokwe.

Hata hivyo wakaazi wa maeneo hayo wanaomba msaada kutoka kwa Shirika la Huduma za Wanyamapori KWS, kuchukua hatua haraka ili kumkamata mnyama huyo.

Subscribe to eNewsletter