Wakaazi wa eneo la Arge,Marsabit walalamikia kile wamekitaja kuwa mnyama anayetisha…
February 24, 2025
NA MUCHAI MUNIU
Mkurugenzi mwandamizi msaidizi wa shirika la wanyama pori KWS tawi la kaskazini mashariki Gideon Kebati amepuuzilia mbali madai ya mnyama anayedaiwa kuonekana katika kaeneo ya Arge wadi ya South Horr.
Kulingana na Kabeti huenda ikawa mnyama huyo ni nyani wala sio sokwe mtu kama inavyodaiwa.
Aidha ametoa hakikisho kuwa KWS inafanya kazi na vitengo mbali mbali ili kuhakikisha kuwa wakaazi wa maeneo hayo wako salama huku akiwatakata wakaazi kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Akiongea na idhaa hii kebati ametoa hakikisho la usalama akiwataka wakaazi kuwa na utulivu kwani hakuna sababu yoyote ya kuwa na hofu. Amesema kuwa aina ya mnyama anayedaiwa kuonekana hupatikana tuu kwenye misitu ya Equitorial kama vile Rwanda na Kongo ila sio hapa nchini Kenya.