Wakaazi wa eneo la Arge,Marsabit walalamikia kile wamekitaja kuwa mnyama anayetisha…
February 24, 2025
NA SABALUA MOSES
Chama cha walimu nchini KNUT tawi la Marsabit kimeitaka serikali kuharakisha kutoa ufadhili wa pesa za kufadhili masomo ili kuhakikisha kuwa shughuli za masomo zinaendlea vilivyo.
Akizungumza na Redio ya Jangwani katibu mkuu wa KNUT tawi la Marsabit Rosaline Talaso amesema kuwa kufikia sasa bado fedha hizo hazijawafikia shule hivyo kutatiza shughuli katika shule mbalimbali hapa jimboni Marsabit.
Talaso pia ameiomba serikali kuongeza fedha hizo ili kuboresha hali shuleni.
Vilevile Talaso amelalamikia Bima ya walimu inayofahamika kama Makel kusitishwa na baadhi ya watoa huduma wa kibinafsi pamoja na tasisi za umma jambo linalemaza zoezi za walimu kupata huduma za afya.
Hata hivyo Bi Talaso ameiomba serikali kusaidia katika kulaiinisha bima ya afya ya SHA ili iweze kusaidia walimu pamoja na wananchi kwa jumla