Local Bulletins

Uzinduzi rasmi wa kampeni ya  chanjo ya polio wafanyika katika hospitali kuu ya Marsabit

Afisa mkuu anayesimamia maswala  ya dharura kwenye sekta ya afya  katika hosptali kuu ya ya rufaa Marsabit Abdi Sora  amesema kuwa kampeni ya chanjo ya ugonjwa huo umezinduliwa leo katika hospitali kuu ya rufaa mjini Marsabit .

Uzinduzi huo ulijumuisha washikadau mbalimbali ikiwemo maafisa wa serikali kuu, serikali ya kaunti, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, WHO, UNICEF pamoja na wizara ya afya

Vile vile Abdi Sora amesema kuwa kampeni hiyo imezinduliwa kwa minajili ya  kupambana na makali ya ugonjwa wa polio  baada ya kisa kimoja  kupatikana katika nchi  jirani ya Ethiopia.

Kampeni hiyo ya OBR1 kulingana na Sora itaendelea kwa muda wa siku tano katika kaunti ya Marsabit pamoja na kaunti nyingine zilizopo  karibu na nchi ya Ethiopia

Aidha Sora amesema kampeni hiyo inalenga watoto wenye chini ya umri wa miaka 11 huku shughuli za hamasisho zikiendelea kufanyika katika kaunti ya Marsabit.

Subscribe to eNewsletter