Vijana wa Saku wamelalamikia serekali ya kaunti ya Marsabit kutoidhinisha maswala waliyoibua wakati wa vikao vya kushirikisha umaa kwenye marekebisho ya bajeti…
February 5, 2025
Na Caroline Waforo,
Wakaazi wa eneo la Kakare Scheme eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wanalalamika kuhangaishwa na simba wawili ambao wanaendelea kuwavamia mifugo wao na hata kuwaua kadhaa katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Ann Letur mmoja wa wakaazi hao amesema kuwa ngombe wake walivamiwa na kuuwawa siku ya Jumamosi iliyopita huku akisalia kuhesabu hasara.
huyo amesema kuwa kwa sasa hata binadamu wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na simba hao.
Kutokana na hilo wakaazi hao wamelitaka shirika la huduma za wanyamapori nchini KWS kuwaondoa simba hao kwa haraka ili wananchi waishi bila wasiwasi.