County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Entertainment, Local Bulletins, National News

NCCK TAWI LA MARSABIT YAWARAI WANANCHI KUDUMISHA AMANI NA UPENDO

Baraza la makanisa nchini NCCK tawi la Marsabit limetoa wito kwa Wakenya kudumisha Amani na upendo.

Kwenye arafa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kusomwa na mwenyekiti wa kanisa la PCEA mjini Marsabit Elijah Kamitha, NCCK imetoa wito kwa wananchi kukumbatia Amani sawa na maelewano ili kueneza upendo katika jamii.

Baraza hilo likitaja kwamba ni jukumu la kila mmoja katika jamii kuhakikisha kwamba Amani inasheni nchini.

Aidha katika ujumbe huo NCCK imelitaja swala la mazungumzo,kuzingatia usawa katika ugawi wa rasilimali sawa na maswala mengine kama njia mwafaka za kuhakikisha kwamba Amani inasheheni kote nchini.

Hata hivyo NCCK imetoa wito kwa wananchi kujiepusha na maswala ya kulipiza kisasi na badala yake kukumbatia mazungumzo ili kutatua mizozo inayojiri katika jamii.

Subscribe to eNewsletter