KITUO CHA KUOKOA WANAOPITIA DHULMA ZA KIJINSIA KUANZISHWA LOGLOGO KAUNTI YA MARSABIT
November 6, 2024
Viongozi wa kidini katika kaunti ya Marsabit wameunga mkono kauli ya rais William Ruto ya kuitaka jamii kuangazia kuhusu maadili mema kwa ajili ya kupunguza visa vya mauaji ya wanawake nchini.
Akizungumza na idhaa hii, mchungaji wa kanisa la Redeemed Gospel hapa Marsabit Silver Savali ameelezea kuwa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kuwa wanao wanafunzwa maadili mema, ambayo yatawasaidia katika kujiepusha na vitendo katili ambayo inahujumu haki ya binadamu.
Pasta Savali amesema kuwa visa hivi vya mauaji ya wanawake nchini vitapungua iwapo jamii itaungana na kuweza kutoa mafunzo sahihi kwa vizazi vya sasa.
Mhubiri Savali amewataka wananchi kuepuka tamaa ya pesa kwani ndio chanzo kikuu cha mauaji haya akisema kuwa wananchi wanafaa kuridhika na walichonacho.
Kauli yake imeweza kuungwa mkono na Imamu wa Msikiti wa Jamia hapa Marsabit, Sheikh Mohammed Noor ambaye amesema kuwa ni wajibu wa kila mzazi kujua mienendo ya wanao na pia kuweza kuwasaidia katika kuwawajibisha nyumbani na hata katika sehemu za dini.
Hata hivo ameichangamoto serekali kuweza kubuni mbinu mbadala ambazo zitasaidia katika kukabiliana na wahuni ambao wanatekeleza mauaji hayo.