Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Zaidi ya watu 50 wamenufaika na vifaa kutoka kwa shirika la The National Fund for the Disabled of Kenya (NFDK) katika kaunti ya Marsabit.
Kwa mujibu wa mwanachama wa bodi ya shirika hilo Profesa Julia Ojiambo ni kuwa watu hao ni kutoka kaunti ndogo tatu za jimbo la Marsabit ambazo ni Laisamis, Saku na Moyale.
Akizungumza katika zoezi la kuwakabidhi watu 17 walionufaika na mpango huo katika kaunti ndogo Saku hii leo,Profesa Ojiambo ametaja kuwa wanalenga kuhakikisha kwamba kaunti zote ndogo hapa jimboni Marsabit zinapata msaada.
Aidha Profesa OJiambo amewataka watu walio na watoto wanaoishi na ulemavu au waliona ulemavu kuchukua fomu na kujiandikisha katika afisa za mabaibu kamishina ili kujisajili na kupata masaada kutoka kwa shirika hilo.
Profesa Ojiambo amewarai wananchi kuasi unyanyapa kwa watu wanaoishi na ulemavu huku akiwataka kutowaficha na badala yake kuhakikisha kwamba wamesajiliwa ili waweze kusaidika.
Amewarai walionufaika na vifaa hivyo kutouza na badala ya kuvitimia kujinufaisha kimaisha.
Kwa upande wao wananchi walionufaika na vifaa pamoja na hundi za pesa kutoka kwa shirika la NFDK wakiongozwa na John Boru Galgallo wamelishukuru shirika hilo huku wakilitaka kuongeza ya idadi ya watu wanaopata msaada kutoka kwao.