County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Entertainment, Local Bulletins, National News

WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.

Wazazi Marsabit wahimizwa kutowaficha watoto walio na ulemavu wa kupooza kwa ubongo maarufu celebral palsy.

Wazazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutowaficha watoto walio na ulemavu wa kupooza kwa ubongo maarufu celebral palsy, hali ambayo huathiri ubongo wa mtoto, mama akiwa mja mzito.

Ni hamasa ambayo imetolewa na mhudumu wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Waqo Huqa.
Kulingana na Huqa kupoozwa kwa ubongo kunasababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo afya ya mama huku akiwaonya akonamama walio na uja uzito dhidi ya unywaji pombe au uvutaji wa sigara kwani unachangia hali hiyo.
Kwa upande wake Millicent Aoro ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ni kuwa wazazi na jamii kwa ujumla wanafaa kuhamasishwa kuhusiana na ugonjwa huu wa kupooza kwa ubongo.
Mhudumu huyo wa afya vilevile ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto wanaougua ugonjwa huu hospitalini kwa ushauri zaidi.

Subscribe to eNewsletter