County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Entertainment, Local Bulletins

MITIHANI WA KITAIFA KCSE WANGOA NANGA,WANAFUNZI 3,748 WAKIKALIA MITIHANI HUO KAUNTI YA MARSABIT….

Idara ya elimu kaunti ya Marsabit imejiandaa kuhakikisha kwamba mitihani ya kitaifa KCSE inaendelea kama ilivyoratibiwa.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa mitihani hiyo imeanza vyema katika vituo vyote 52 vya mitihani hapa jimboni.

Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisini mwake,Magiri ameweka wazi kuwa mikakati kabambe imewekwa ikiwemo ndege ya kusafirisha mitihani iwapo kutashuhudiwa mvua.

Aidha Magiri ametaja kwamba kuna kituo kimoja ya wanafunzi wa kibinafsi (Private Candidates) ambapo watahiniwa 157 wanakalia mitihani huo katika shule ya msingi ya St Theresa hapa mjini Marsabit.

Hata hivyo Magiri amewaonya wasimamizi wa mitihani hiyo kutojihusisha na visa vya udanganyifu kwani watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mkuu huyo wa elimu jimboni amesisitiza kwamba idara ya elimu itawabadilisha wasimamizi wa mitihati kila wiki ili kuzuia visa vya udanganyifu.

Mwaka huu unashuhudia idadi kubwa ya wasichana wanaokalia mtihani huo ambao ni 1,883 ikilinganaishwa na wavulana 1,765.

Hata hivyo mtahiniwa mmoja anakalia mtihani wake katika rumande ya hapa mjini Marsabit baada ya kutiwa mbaroni.

Subscribe to eNewsletter