County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

MARSABIT IMEELEKEA KIKAMILIFU KWA AJILI YA KIPINDI CHA UKAME – ASEMA WAZIRI WA KILIMO HUSSEIN ALI FUNDI.

Kaunti ya Marsabit imejiandaa kikamilifu ili kuhakikisha kwamba wananchi hawaadhiri zaidi katika kipindi cha ukame kame ilivyo shuhudiwa miaka ya nyuma.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa kilimo katika kaunti ya Marsabit Hussein Ali Fundi.

Akizungumza na waandishi wa habari hapa mjini Marsabit, waziri Fundi ametaja kwamba kwa sasa idara hiyo imewekeza katika kukusanya maji yanayoweza kutumika wakati wa kiangazi katika kila wadi huku wafugaji 6,000 wakiwachukulia mifugo wao bima.

Hata hivyo waziri Fundi ametaja kwamba idara ya kilimo hapa jimboni imeweka mikakati dhabiti kuzuia mzozo wa malisho kati ya wafugaji wa hapa jimboni Marsabit na kaunti jirani.

Waziri Fundi amekariri hoja ya wakulima kuangazia kilimo cha kunyunyuzia maji ili kuhakikisha kwamba kaunti ya Marsabit inajiweka kando na hatari ya ukosefu wa chakula.

Subscribe to eNewsletter