WAKAAZI WA MARSABIT WAONESHA MATUMAINI YA KESI ZAO KUKAMILISHWA HARAKA NA MFUMO WA AJS
November 22, 2024
FAIDA inayopatikana kwa kuuza bidhaa za Moyale Kenya kwenda Ethiopia imetajwa kupungua kutokana na kushuka kwa thamani na kudidimia kwa sarafu ya Ethiopia Birr.
Naibu Mwenyekiti wa chama cha wanabiashara KNCCI tawi la Marsabit Alinur Mumin ameambia shajara kuwa kushuka kwa nguvu ya sarafu hiyo imeteremsha faida na mchakato mzima wa biashara katika mji huo wa mpakani.
Alinur pia ametaja vichorochoro vingi mpaka pale ambavyo vimefanya kituo kikuu cha forodha ya One Stop Boarder Post kutotumika sana.
Suala lingine linalofanya kituo hicho kutotumika sana ni ushuru unaotozwa bidhaa ambayo anataja kuwa ya juu na hivyo wafanyabishara kuikwepa.
Ametaja haja ya serikali kupitia wizara ya Biashara na Hazina kuu kuendesha elimu kuhusu umuhimu wa kulipa ushuru.
Aidha amelalamikia kiwango cha juu cha malipo ya kupata nguvu za umeme suala analosema inalemaza biashara.