County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins, National News

IDARA YA MISITU KAUNTI YA MARSABIT INALENGA KUPANDA MITI KATIKA MAENEO KAME.

Idara ya misitu humu jimboni Marsabit inalenga kupanda miti katika maeneo kame, tambarare na milima humu jimboni ili kupunguza maeneo yenya jangwa pamoja na kufanikisha mpango wa seriklai wa kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2032 ambapo kaunti ya Marsabit imeratibiwa kupanda miti bilioni 2.5 ifikapo mwaka huo.

Mradi huu utafanikishwa na wataamlam kutoka nchini Israeli na utafadhiliwa na benki kuu ya Dunia Kwa ushirikiano na serikali kuu kupitia idara ya msitu nchini.

Mradi huu ambao utafanikishwa katika kaunti tano zinazojumuisha kaunti ya Marsabit, Isiolo, Samburu, Turkana na Wajir utaanza kutekelezwa mapema mwakani.

Akizungumza na shajara ya radio jangwani mhifadhi wa msitu jimboni Mark Lenguro amesema kuwa miche itakayopandwa ina uwezo wa kufanya vizuri katika maenneo kame.

Mark anasema kuwa miti hiyo itapandwa kutumia ndege spesheli.

Aidha Mark amesema lengo lao sio kupunguza maeneo jangwa yanayovutia watalii jimboni kama vile Chalbi Desert bali ni kupunguza kuenea kwa maeneo hayo.

Aidha amesema kuwa kufanikishwa kwa mradi huo kutawawezesha wananchi kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa nyuki.

Lenguro kadhalika amesema kuwa mradi huo pia utatoa nafasi za ajira kwa wakaazi jimboni

Iwapo mradi huu utafanikishwa utasaidia pakubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Subscribe to eNewsletter