County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

HIFADHI YA MELAKO IMETAJA KWAMBA KAMWE HAIMUJUI JAMAA ALIYEUWAWA AKIWA AMEVALIA JAKETI YA ZAMANI YA HIFADHI HIYO MNAMO SIKU YA IJUMAA WIKI ILIYOPITA KATIKA ENEO LA BADASA ENEO BUNGE LA SAKU KAUNTI YA MARSABIT.

 Hifadhi ya Melako imetaja kwamba kamwe haimujui jamaa aliyeuwawa akiwa amevalia jaketi ya zamani ya hifadhi hiyo mnamo siku ya ijumaa wiki iliyopita katika eneo la Badasa eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit.

Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia simu Meneja wa hifadhi ya Melako Satim Eydimole ni kuwa hawamjui jamaa huyo na hajawahi fanya kazi na hifadhi ya Melako kwani hayupo hata kwenye rekodi zao za wafanyikazi wazamani.

Aidha Satim ametaja kwamba msimamo wa hifadhi ya Melako ni kuwa wao ni bado ni mabalozi wa Amani na kwamba kamwe hawataruhusu walio na njama ya kuvuruga amani inayozidi kushuhudiwa hapa jimboni kutatizwa na wahuni fulani.

Hata hivyo Satim ameja kwamba usimamizi wa hifadhi hiyo chini ya uangalizi wa OCS wa eneo la Laisamis uliandaa zoezi la ukaguzi wa mavazi ya maskauti wao wote ili kuhakikisha kwamba hakuna yeyote amepoteza wala kuazima mtu vazi lake.

Subscribe to eNewsletter