County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

JAMII YA MARSABIT YATAKIWA KUTOWAFICHA WATU WANAOISHI NA ULEMAVU NA BADALA YAKE KUWALINDA.

Na JB Nateleng,

Naibu kamishna wa Marsabit ya Kati David Saruni ametoa wito kwa jamii ya Marsabit kutowaficha watu wanaoishi na ulemavu na badala yake kuwalinda na kuwatunza kama watu wengine.

Saruni amesema kuwa wakazi wa Marsabit wanafaa kuasi Mila potovu inayowadunisha watu wanaoishi na ulemavu kwa sababu imepitwa na wakati.

Ameeleza kuwa serekali kuu inawajali watu wanaoishi na ulemavu hata kupitia bima mpya ya afya SHIF

Afisa mkuu katika idara ya tamaduni,jinsia na huduma za jamii katika kaunti ya Marsabit Anna Maria Deng’e amewataka akinamama kuwapeleka wanao katika zahanati iliyopo karibu iwapo watajifungua mtoto aliye na kasoro ili kuzuia ulemavu.

Subscribe to eNewsletter