Rais Ruto asikitikia hali ya usalama nchini DRC haswa ukanda wa unaokaliwa na waasi wa M23.
January 27, 2025
Na Isaac Waihenya & Abdilaziz Abdi,
Ni aslimia 30 pekee ya watu wanaoishi katika miji ya Marsabit wanapata maji safi ya matumizi.
Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu katika idara ya maji hapa jimboni Marsabit Rob Galma.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee wakati wa hafla ya kutolewa kwa data zilizokusanywa na shirika la M-Water na ambazo zinaonyesha kiwango cha vyanzo vya maji katika kaunti ya Marsabit, Galma amesema kuwa angalau asilimia 70 ya watu wanaoishi vijijini katika kaunti ya Marsabit wanapata maji safi ya matumizi.
Aidha Galma amesema kuwa watatumia data hizo walizopata kutoka kwa shirika la M-Water kupanga mikakati ya namna ya kuogeza idadi ya watu wanaopata maji hapa jimboni.
Hata hivyo Galma ameweka wazi kuwa jimbo la Marsabit lina vyanzo vya maji 650 huku asilimia 62 ya vyanzo hivyo vikiwa vinafanyakazi.
Ametaja kwamba idara ya maji kaunti ya Marsabit inalenga kuongeza kiwango hicho ili kuhakikisha kuwa WanaMarsabit wanapata maji safi ya kunywa na ya matumizi.