Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

TUKUMBATIE TEKNOLOJIA MARSABIT ILI KUBORESHA UJUZI NA KUWAPA AJIRA VIJANA. – ASEMA MKURUGENZI WA MKAHAWA WA EBISA MARSABIT, ABDIKADIR DOYO WARIO

Na JB Natelng,

Suala la Teknolojia linafaa kuangaziwa kwa undani katika kaunti ya Marsabit ili kuboresha ujuzi wa vijana ambao mara nyingi hujikuta mtaani bila ajira.

Haya yamekaririwa na mkurugenzi wa mkahawa wa Ebisa  hapa mjini Marsabit, Abdikadir Doyo Wario.

Akizungumza na wanahabari baada ya kutoa hamasa kwa vijana kuhusu teknolojia, Wario amesema kuwa upungufu wa vifaa pamoja na wakufunzi ambao watawasaidia vijana kuelewa teknolojia vyema ndio umechangia katika ukosefu wa kazi jimboni.

Wario ameelezea kuwa vijana katika kaunti ya Marsabit huwa wanakosa kupata taarifa muhimu kuhusu nafasi za kazi ambao huwa zinatangazwa mitandaoni kwa sababu ya kukosa uelewa wa matumizi bora ya mitandao.

Hata hivo amewashauri vijana kufika katika kituo kipya cha mafunzo katika mkahawa wa Ebisa ili kuweza kupata mafunzo na pia jinsi ya kutumia mtandao kujiboresha na kujitaftia riziki.

Subscribe to eNewsletter