HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
.
Na Isaac Waihenya,
Onyo kali imetolewa kwa kliniki za kibinafsi mjini Marsabit dhidi ya kutotupa vifaa vilivyotumika vya matibabu kwa njia isiyofaa.
Onyo hii imetolewa na afisa wa afya katika kaunti ndogo ya Saku Daktari Duba Doyo Abduba, ambaye ametaja kwamba kumekuwepo na ongezeko la vifaa vya kimatibabu ambavyo vimetapakaa ovyo mjini na hata vijijini.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Daktari Doyo ametaja kwamba hilo linahatarisha Maisha ya wanaMarsabit huku akionya wale wanaoendeleza tabia hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria au hata kunyanganywa leseni za kuhudumu hapa jimboni Marsabit.
Aidha Daktari Doyo amezitaka kliniki za kibinafsi kuzingatia taratibu zilizowekwa na wizara ya afya katika kutupa au kuchoma vifaa hivyo ili kulinda afya ya jamii.