Highlights

Wazazi watakiwa kufuatilia watoto wakati wa likizo fupi ya muhula wa pili

Na Joyce Akinyi & JB Nateleng

Huku wanafunzi wakitarajiwa kurejea nyumbani kwa likizo fupi ya muhula wa pili wiki hii, wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kufuatilia kwa karibu shughuli wanazojihusisha nazo wakiwa nyumbani.

Wito huo umetolewa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi na sekondari ya St. John’s Boru Dabasso, ambaye amesema ni muhimu kwa wazazi kuwafuatilia watoto wao ili kuwazuia kujiingiza katika makundi yasiyofaa yanayoweza kuwashawishi kutumia dawa za kulevya na hivyo kuharibu maadili yao.

Aidha, amewahimiza wanafunzi kutumia vyema kipindi cha likizo kwa kujisomea na kudurusu, sambamba na kuwasaidia wazazi katika shughuli za nyumbani.

Dabasso ameyasema hayo katika hafla iliyowakutanisha pamoja wanafunzi kutoka shule za St. Teresa girls , St. John’s Memorial, Little Angels na AIC, ambapo walishiriki mashindano ya michezo ya kuchaguliwa kwa timu bora itakayoshiriki mashindano ya muhula wa pili kwa shule za msingi na sekondari msingi katika kaunti ndogo ya Marsabit Central yatakayofanyika mwezi ujao.

Post Comment