Highlights

Wakazi wa Badanrero walalamiki ukosefu wa maji

Na Sabalua Moses

Wakazi wa eneo la Bada Rero wamelalamikia ukosefu wa maji, hali ambayo imeathiri shughuli za nyumbani na ufugaji, na kuwafanya wakazi kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Wakizungumza na Radio Jangwani kupitia simu, baadhi ya wakazi wamesema changamoto ya maji imekuwa ya muda mrefu, na sasa inahitaji suluhisho la haraka kutoka kwa mamlaka husika.

Hata hivyo, chifu wa eneo hilo Dida Galgalo amesema kuwa kwa sasa hali iko shwari, akibainisha kuwa Bada Rero ina visima vya kutosha vinavyoweza kuhudumia wakazi wote endapo vitasimamiwa ipasavyo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment