Highlights

Watu wanaoishi na ulemavu wametakiwa kujisajili kama wapiga kura

Na Sabalua Moses

Huku zoezi la usajili wa wapiga kura likiendelea, watu wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Marsabit wamehimizwa kujitokeza kutafuta vitambulisho vya kitaifa na kujisajili kama wapiga kura.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani, mwenyekiti wa chama cha watu wanaoishi na ulemavu, Dokata Kuro, amesema kuna haja ya kuwafikia watu wanaoishi mashinani ili kuhakikisha wanapata fursa ya kusajiliwa na kufanya maamuzi wakati wa uchaguzi.

Aidha, Dokata amesema watu wanaoishi na ulemavu wanapaswa kujumuishwa katika shughuli za tume ya uchaguzi IEBC pamoja na vyama mbalimbali vya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kushiriki kama maajenti wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kundi hilo linahitaji uwakilishi maalum katika serikali za kaunti na pia katika serikali ya kitaifa ili kuhakikisha maslahi yao yanazingatiwa.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment