Highlights

Wakazi wafunga kituo cha afya Manyatta Jillo wakilalamikia huduma duni.

Na Abdilaziz Yusuf

Wakazi wa eneo la Manyatta Jillo eneobunge la Saku wamefunga kituo cha afya cha eneo hilo wakilalamikia huduma duni ambazo, kwa mujibu wao, zimeendelea kwa muda mrefu.

Wakazi hao wanasema wamechoshwa na ukosefu wa wahudumu wa afya, hasa wauguzi waliodaiwa kuhamishwa na kuacha kituo hicho bila huduma za kutosha.

Aidha, wakazi hao wamedai kuwa wamejaribu mara kadhaa kuwasilisha malalamiko yao kwa serikali bila mafanikio, hali iliyowalazimu kuchukua hatua ya kufunga kituo hicho.

Sasa wanatoa wito kwa idara ya afya pamoja na serikali ya kaunti kuingilia kati haraka iwezekanavyo, kuboresha huduma na kuhakikisha wauguzi waliotolewa wanarejeshwa.

Hata hivyo, juhudi za kupata maoni kutoka kwa maafisa wa afya wa kaunti bado hazijafanikiwa kufikia sasa.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment