Washukiwa wa pembe za ndovu wakana mashtaka Marsabit
Washukiwa watatu waliokamatwa na pembe za ndovu zenye uzito wa kilo 39.5 mnamo tarehe 11 Juni katika eneo la Majengo, kaunti ya Marsabit, wamekana mashtaka ya kumiliki pembe hizo kinyume cha sheria.
Mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Marsabit, Edward Oboge, washukiwa hao ambao ni Umuro Afani Duba, Halkano Elema na Wario Ali Halo, wametakiwa kulipa bondi ya shilingi milioni tatu kila mmoja.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 13 Julai kabla ya kuanza kusikilizwa tarehe 27 Julai mwaka huu.



Post Comment