Highlights

Marsabit Mix wang`ara kwenye Voliboli Saku, huku Moi Girls wakiendelea kututea ubingwa wao.

Na JB Nateleng

Mashindano ya michezo ya shule za sekondari katika kaunti ndogo ya Marsabit Central yameendelea kushuhudia ushindani mkali huku timu mbalimbali zikitawazwa mabingwa katika fani tofauti.

Katika mpira wa Voliboli kwa wavulana Shupe ya Marsabit Mix ilitawazwa mabingwa baada ya kuifunga Shule ya Badassa Senior seti tatu kwa bila katika mchezo wa fainali uliovutia mashabiki wengi.

WhatsApp-Image-2026-06-20-at-14.53.15-e1781965427478-1024x461 Marsabit Mix wang`ara kwenye Voliboli Saku, huku Moi Girls wakiendelea kututea ubingwa wao.
Wachezaji wa Voliboli wa Moi Girls

Kwa upande wa mpira wa voliboli kwa wasichana, Moi Girls iliibuka mabingwa baada ya kuichapa Dakabaricha kwa seti tatu kwa bila na kutwaa taji la ubingwa.

Katika kandanda ya wasichana, Moi Girls iliendeleza ubabe wake kwa kuwalaza Sasura Girls mabao 3-0 na kutwaa ubingwa huo ambao uliashiria kuwa wako ange kutetea ubabe wao kwa masuala ya kandanda Marsabit Central.

Moi Girls pia waliongeza taji lingine katika mchezo wa netiboli baada ya kuibuka washindi dhidi ya Marsabit Mix. kwenye shindano hilo Moi girls waliweza kuilaza Marsabit Mix bao 30 – 9 na hivyo kujinyakulia ubingwa wa mashindano hayo.

Timu zilizotwaa mataji katika mashindano haya zinatarajiwa kuwakilisha kaunti ndogo ya Marsabit Central katika mashindano ya ngazi ya Kaunti yatakayofanyika mwezi wa Julai.

Kwingineko kwenye kandanda ya wavulana, shule ya upili ya Dakabaricha na Badassa Senior School zimefuzu kwa fainali ya kandanda ya wavulana katika mashindano ya KSSSA Marsabit Central baada ya kuibuka washindi katika michezo yao ya nusu fainali.

Dakabaricha ilijikatia tiketi ya kucheza fainali baada ya kuichapa shule ya upili ya Gadamoji mabao 2-1 katika mechi ya kusisimua iliyoshuhudia ushindani mkubwa kutoka kwa timu zote mbili.

726660360_2231215514301813_8564095699031566997_n-1024x771 Marsabit Mix wang`ara kwenye Voliboli Saku, huku Moi Girls wakiendelea kututea ubingwa wao.
Wanafunzi wa shule ya upili ya Badassa wakisakata kandanda katika uwanja wa Dakabaricha

Katika nusu fainali nyingine, Badassa Senior School iliibuka mshindi kwa bao 1-0 dhidi ya shule ya upili ya Gororukesa na hivyo kufuzu kwa fainali.

Matokeo hayo sasa yanaweka mazingira ya fainali kali kati ya Dakabaricha na Badassa Senior School, huku timu zote zikisaka taji la ubingwa wa kandanda ya wavulana wa Marsabit Central.

Post Comment