El-Mosaretu Girls Yang’ara katika Tamasha la Muziki la Kaunti ya Marsabit
Na JB Nateleng
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya El-Mosaretu imeikuwa miongoni mwa shule zilizofanya vyema zaidi katika tamasha la muziki la kaunti ya Marsabit lililofanyika katika Shule ya Moi Girls kuanzia Alhamisi 18 Juni na kuhitimishwa Jana Ijumaa Juni 19. Shule hiyo ilijizolea ushindi katika vipengele kadhaa, ikiwemo nafasi ya kwanza katika Equity Choral, Solo Verse ya Kidato cha Nne, wimbo wa Kiturkana na Ngoma ya Kiturkana.
Mbali na ushindi huo, El-Mosaretu Girls ilipata nafasi ya pili katika Choral Verse, Solo Verse ya Gredi ya Kumi, Shairi, Wimbo wa Kisamburu na Ngoma ya Kisamburu. Shule hiyo pia ilishika nafasi ya nane katika kipengele cha Turkana Sacred Song, matokeo hayo yakionyesha ukuaji wa vipaji vya muziki, sanaa na utamaduni miongoni mwa wanafunzi wa El- Mosaretu.

Mafanikio hayo yamehusishwa na juhudi za uongozi wa mwalimu mkuu Madina Woche, pamoja na mwalimu wa muziki Tchabu Marcelino, ambao wamekuwa wakisimamia maandalizi ya wanafunzi kwa mashindano mbalimbali.
El-Mosaretu Girls, iliyoko Loiyangalani, ilianzishwa mwaka 2023 na Shirika la Kenya Dryland Education Fund (KDEF) kwa lengo la kuwapa wasichana kutoka jamii za wafugaji fursa sawa za elimu na maendeleo.



Post Comment