Wanasiasa waonywa dhidi ya lugha ya chuki Marsabit
Na Abdiazizi Yusuf & Nyabande Orwa
Huku dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matamshi ya chuki, naibu mwenyekiti wa kamati ya amani Marsabit, Adan Chukulisa, amewataka wakazi na viongozi kushirikiana ili kuhakikisha amani iliyodumu kwa muda mrefu katika kaunti hiyo inaendelea kudumishwa.
Chukulisa amesema huu ni wakati mwafaka kwa wanasiasa wanaojiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao kuwa waangalifu katika matamshi yao ili kuepuka kauli zinazoweza kuleta migawanyiko miongoni mwa jamii mbalimbali za Marsabit.
Wakati huo huo, amewahimiza wananchi kuendeleza umoja na mshikamano, huku akiwaonya dhidi ya viongozi wanaotumia lugha ya chuki na kuwachochea wananchi kugawanyika.
Naye…. wakaazi wa kaunti ya Marsabit wameitaka serikali kuonyesha usawa katika mapambano dhidi ya matamshi ya chuki nchini.
Wakaazi hao wamesema kuwa hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaotoa matamshi ya chuki zinaonekana kutegemea upande wa kisiasa anaotoka mhusika.
Baadhi yao wanadai kuwa viongozi na watu walio upande wa upinzani huchukuliwa hatua wanapotoa matamshi chuki ilhali wale walio serikalini mara nyingi hawaadhibiwi kwa makosa kama hayo.



Post Comment