Wakulima wa eneo la Manyatta koso ,Dakabaricha Marsabit walalamikia kero la nyani.
Na Sabalua Moses
Wakulima kutoka eneo la Dakabaricha , manyatta Koso Marsabit central wanakadiria hasara katika mashamba yao kufuatia nyani wanaoharibu mimea yao shambani .
Akizungumza na shajara ya radio jangwani mkulima Waqo Woche amesema kuwa mara nyingi nyani hao huharibu mahindi na paipai jambo ambalo linadunisha mazao yao shambani
Kwa upande wake Guyo Urthulo ambaye pia ni mkulima katika eneo hilo pia anatoa wito kwa idara ya kuwalinda Wanyama pori KWS kuhakikisha kuwa wanawadhibiti Wanyama hao.



Post Comment