Polisi watoa hakikisho la usalama kwa maandamano ya AlhamisiĀ Marsabit.
Na Nyabande Orwa
Kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, amesema kuwa idara ya usalama iko tayari kutoa ulinzi wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii.
Akizungumza na kituo hiki ofisini mwake, Kimaiyo amesema maafisa wa usalama watakuwa kazini ili kuhakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa utulivu na usalama.
Hata hivyo, amewataka vijana hao kuandamana kwa amani, kuepuka kuharibu mali ya umma na ya watu binafsi, na kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya utaratibu kisha kurejea makwao.
Kauli yake inajiri huku Rais William Ruto akiwa amewahimiza vijana wanaotarajia kushiriki maandamano hayo kufanya hivyo kwa amani na kwa kuzingatia sheria, wanapowaenzi wale waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya mswada wa fedha 25 Juni mwaka 2024.



Post Comment