Wanafunzi 4,000 hajaripoti shuleni kutokana na athari za kiangazi, Marsabit
NA JB Nateleng
Wanafunzi 4,000 wamefeli kuripoti shuleni kutokana na athari za kiangazi katika kaunti ya Marsabit.
Haya yamebainika wakati wa kikao cha kamati ya kutathmini majanga katika kaunti ya Marsabit (CSG) ambapo wito umetolewa kuangazia athari za ukame mashuleni ili kusaidia wanafunzi kusalia shuleni na kuwatafuta wale ambao hawajarejea.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa Mamlaka ya kukabili Majanga na Ukame (NDMA), tawi la Marsabit Guyo Golicha, amesema kwamba hali hiyo imechangiwa na familia kuhama kutafuta malisho na maji katika maeneo ya mbali, jambo linalosababisha watoto kukosa kutorejea shuleni.



Post Comment