Highlights

Wakazi wa Moyale na Dukana wanufaika na msaada wa chakula kutoka serikali kuu

NA Nyabande Orwa

Serikali kuu imetoa chakula cha msaada kwa wakazi wa eneo bunge la Moyale walioathirika zaidi na baa la njaa kutokana na ukame unaoendelea. Hayo yamethibitishwa na naibu kamishna wa Moyale, Benedict Munyoki.

Akizungumza na kituo hiki, Munyoki amesema machifu wamepewa jukumu la kutambua familia zilizoathirika zaidi katika vituo 60 vilivyobainishwa ndani ya eneo hilo. Amesema kwa sasa wakazi watapokea mchele, huku wakisubiri msaada zaidi wa chakula cha mifugo na aina nyingine za chakula kwa binadamu.

Aidha, Munyoki amesema ukosefu wa mvua umesababisha visima vingi kukauka, hali iliyowalazimu wafugaji wengi kuhama hama wakitafuta maji na malisho.

Wakati uo huo katika eneo la Dukana familia 1,500 zimenufaika na chakula cha msaada. Kulingana na naibu kamishna wa eneo hilo Peter Kimani Maina chakula hicho kilitolewa wiki mbili zilizopita na serikali kuu. Kuhusiana na malisho ya mifugo,Maina anasema kuwa kuna nyasi ya kutosha.

Post Comment