Jamii za wafugaji Marsabit zahimizwa kuasi ukeketaji na badala yake kuwapa wasichana elimu
NA Sabalua Moses
Jamii za wafugaji katika kaunti ya Marsabit zimeendelea kuhimizwa kuasi ukeketaji wa mtoto msichana na badala yake kuhakikisha kuwa anapata haki ya elimu.
Wito huu umetolewa na mwanachama wa Shirika la Meriso Women Initiative, Alice Lesepen ambaye amesema kuwa kuwapa wasichana nafasi ya kusoma ni hatua muhimu katika kupambana na mila potovu kama ukeketaji.
Akizungumza na kituo hiki Lesepen amesema kuwa akina mama wanapaswa kuwa kati mstari wa mbele kuwapa wasichana mazingira na fursa zinazohitajika kutimiza ndoto zao kupitia masomo.
Vile vile Alice amesema kuwa kuna haja ya kuzingatia usawa wa kijinsia ili kuhakikisha watoto wote wanapa haki sawa ya elimu.
Aidha ameeleza kuwa mila zilizopitwa na wakati bado ni vikwazo vinavyodhoofisha juhudi za kupambana na ukeketaji na ndoa za mapema katika jamii za wafugaji.



Post Comment