Highlights

Wakazi wa Marsabit central wahimizwa kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo

Na Nyabande Orwa

OCPD wa Marsabit central, Beethoven Gachago, ametoa wito kwa jamii za wafugaji kuendelea kuishi kwa amani na kushirikiana kwa ajili ya maendeleo.

Akizungumzia mkutano wa amani uliofanyika Segel wiki iliyopita, Gachago amesema jamii mbili za wafugaji zinazoishi Marsabit zilikubaliana kuendelea kutumia maeneo ya malisho kwa amani na kwa manufaa ya wote.

Gachago amewahimiza wakazi kutatua migogoro yao kwa njia za amani badala ya kutumia vurugu. Mkutano wa Segel uliwakutanisha viongozi wa usalama, viongozi wa jamii na wanachama wa umma.

Mikutano hiyo imefuatia shambulizi lililotokea mwezi Mei katika eneo la Kambinye, ambapo watu wasiojulikana waliwashambulia wafugaji, na kusababisha vifo vya ngamia wanne huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment