Highlights

Wakazi wa Loglogo wafurahia uzinduzi wa Makao mpya ya kusaidia watoto waliokumbwa na dhuluma

NA JB Nateleng

Wakazi wa Log Logo, eneo bunge la Laisamis, kaunti ya Marsabit, wameeleza furaha yao kufuatia uzinduzi rasmi wa makao ya kuwasaidia watoto waliokabiliana na dhuluma za kijinsia, ikiwemo ukeketaji na ndoa za mapema.

Wakizungumza na idhaa hii, wakazi wamesema kuwa kituo hiki kitawapa watoto waliopitia dhuluma mahali salama na safi, na pia kitasaidia kupambana na mila potovu inayowaathiri watoto, hasa wasichana. Wameisisitiza pia umuhimu wa kuendeleza mafunzo kwa jamii ili wajue faida ya kituo hicho.

Kwa upande wake, Eunice Baselle amesema hadi sasa kituo hicho kimepokea waathiriwa 24, na kusisitiza haja ya kuongeza vyumba kutokana na idadi kubwa ya waathiriwa. Pia amewataka wahisani kuunga mkono ujenzi wa vyumba zaidi.

Aidha, Eunice ameitaka jamii kuheshimu haki za mtoto msichana na kumruhusu kufanya maamuzi yanayomsaidia kujikuza kimaisha.

Post Comment