IPOA yaanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha Liban Charfi kufuatia malalamishi ya wananchi
NA Caroline Waforo
Mamlaka ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi IPOA imeanzisha uchunguzi kubaini iwapo maafisa wa polisi walihusika katika kisa cha kutoweka kwa Liban Boru Charfi tarehe 25 Januari mwaka 2026, ambaye baadaye alipatikana ameuwawa na mwili wake kutupwa katika eneo la Yashareh eneobunge la Moyale.
Hii ni kufuatia malalamishi kutokwa kwa wananchi, kuhusu tuhuma za kuhusika kwa maafisa wa polisi katika kisa hicho.
Duru za kuaminika zimeaarifu meza ya Shajara kuwa maafisa wa IPOA tayari wamewasili katika eneobunge la Moyale kuchunguza madai hayo.
Siku ya hapo jana Jumapili wakaazi wa Moyale walishiriki maandamano kukashifu mauaji ya Charfi pamoja na misururu ya utekaji nyara katika eneo hilo.
Wakaazi hao pia waliibua madai kwamba, vijana kadhaa wametoweka tangu kuanza kwa operesheni Ondoa Jangili inayoendelea katika eneo hilo.



Post Comment