Jamii ya Marsabit yatakiwa kukomesha dhulma dhidi ya watoto
NA JB Nateleng
Jamii ya Marsabit imetakiwa kukomesha dhulma dhidi ya watoto kwani ni suala linalochangia matatizo ya akili.
Haya yamewekwa wazi na mtaalam wa afya ya akili Sammy Lenawalchingei aliyezungumza wakati wa uzinduzi wa makao salama ya watoto katika eneo la Loglogo eneobunge la Laisamis.
Lenawalchingei ameelezea kuwa, tamaduni zilizopitwa na wakati kama vile ndoa za mapema na ukeketaji, zinachangia msongo wa mawazo miongoni mwa waathiriwa na hata kuwapelekea kujiingiza kwenye matumizi ya mihadarati na dawa za kulevya.
Vile vile ameichangamoto serikali kuu kwa ushirikiano na ile ya kaunti ya Marsabit kujenga kituo cha urekebishaji tabia katika jimbo hili.



Post Comment