DCI wanachunguzi mauaji ya Liban Charfi aliyepatikana ameuwawa baada ya kutoweka, Moyale
NA Caroline Waforo
Idara ya upelelezi katika kaunti ya Marsabit imesema kuwa inachunguza mauaji ya Liban Boru Charfi, mwanaume aliyepatikana ameuawa katika eneo la Yashareh eneo bunge la Moyale baada yake kudaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana.
Afisa mkuu wa upelelezi katika kaunti ya Marsabit Kennedy Nyagah amesema kuwa watu kadhaa wameandikisha taarifa kuhusiana na kisa hicho.
Kulingana naye, uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa Charfi aliuwawa kwa kunyongwa huku pia akiwa na majeraha ya kisu begani.
Nyagah amewataka wananchi walio na taarifa kuhusiana na kisa hicho kuripoti kwa vyombo vya usalama.
Ameihakikishia familia ya marehemu kuwa uchunguzi utakamilika na waliohusika watachukuliwa hatua kali za sheria.
Hapo jana viongozi, wananchi pamoja na familia ya Charfi walikashifu mauaji hayo pamoja na misururu ya visa vya utekaji nyara katika eneobunge la Moyale.
Ali Dulacha mzee kutoka eneo hilo ameitaka serikali kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina umefanyika na hatua kuchukuliwa.
Mwakilishi wadi wa Golbo Edin Adhi ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa vijana wote waliotoweka kwa njia tatanishi wameachiliwa kwa famili zao ima hai au wafu.
Wiki hii seneta wa kaunti ya Marsabit Mohamed Chute aliitaka Wizari ya Usalama wa Kitaifa kuchunguza kifo hicho.
Katika barua kwa Waziri Kipchumba Murkomen, Seneta Chute aliitaka wizara ya Usalama kuwachukulia hatua waliohusika na mauaji hayo huku akiitaka serikali kukabiliana na changamoto za kiusalama katika eneo hilo



Post Comment