Highlights

Kituo cha kuwanusuru watoto chazinduliwa Loglogo

NA JB Nateleng

Kituo cha kwanza cha kuwanusuru watoto wanaokabiliana na dhulma za kijinsia, ikiwemo ukeketaji na ndoa za mapema kimezinduliwa leo Ijumaa katika eneo la Loglogo eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit.

Kulingana na Alicia Leseper ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hicho amesema kwamba ndoto ya kuanzisha kituo hicho kwa jina Loglogo Rescue Centre ilianza mwaka wa 2015 ambapo walitambua shida zinazowakumba watoto wa kike.

Alicia ameelezea kwamba kituo hicho kitasaidia katika kuwasaidia wasichana waathiriwa wa mila na tamaduni zilizopitwa na wakati.

Alicia amedai kwamba ukosefu wa makao salama kama haya unasababisha mwathiriwa kukosa haki.

Vilevile ameitaka jamii kutowatenga wasichana wanaopata mimba.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment