KUPPET yaitaka serikali kuu kuharakisha mchakato wa kupandisha vyeo walimu na kupunguza muda wa kutekeleza CBA.
NA Samuel Kosgei
Katibu wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET Sarr Galgalo ameahidi kuwa ataendelea kupigania maslahi ya walimu wote katika kaunti ya Marsabit.
Mwalimu Galgalo akizungumza baada ya kuchaguliwa tena kuwa katibu wa chama hicho kwa miaka mingine mitano, amewataka walimu kufanya kazi yao kwa ujasiri na kuripoti pindi tu wanapopitia dhulma yoyote.
Kwa upande wake katibu wa Kitaifa wa Masuala ya Uratibu wa Chama cha KUPPET Paul Ngige, ameahidi walimu kuwa muungano wao utasukuma serikali kuipa tume ya kuajiri walimu TSC mgao mkubwa wa kifedha ili kusaidia katika mchakato wa kupandisha vyeo walimu.
Aidha Mainge amelalamikia makato makubwa yanayotekelezwa na serikali kwenye mshahara wa walimu suala analosema inapunguza pakubwa mshahara wa walimu. Hivyo, anaitaka serikali kuharakisha kutekelezwa kwa mkataba wa makubaliano CBA walioandikishana na viongozi wa walimu.
Uchaguzi huo ambao haukuwa na ushindani wowote umefanyika mjini marsabit na kushuhudia wagombea 14 wakisalia mamlakani baada ya kukosa washindani.
Sarr Galgalo amesalia kuwa katibu, Boru Adhi Jattani akiwa mwenyekiti na Wario Roba akiwa mweka-hazina kati vya viongozi wengine.



Post Comment