Highlights

Ukurr Yattani awaonya viongozi wa nje kuingilia siasa za Marsabit

NA Nyabande Orwa

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Marsabit, Ukur Yattani, ametoa wito kwa viongozi wa kaunti jirani kuacha kuingilia siasa za Marsabit.

Akizungumza katika hafla ya kuchangisha pesa za ujenzi wa kituo cha elimu ya kiislamu cha Dakabaricha, Yattani amesema siasa za Marsabit ni tofauti na kaunti nyingine na wakazi wake wana uhuru wa kuchagua viongozi wanaowafaa. Kauli yake ilionekana kuwalenga baadhi ya viongozi kutoka nje ya kaunti, akiwemo mbunge Mishi Mboko, Seneta wa Lamu Joseph Githuku Kamau na mbunge wa Wajir.

Wakati huo huo, Yattani amewataka wanasiasa wanaowania viti katika uchaguzi mkuu ujao kutanguliza amani kwa manufaa ya umoja na maendeleo ya kaunti. Ameahidi kuwaleta pamoja wagombea wa ugavana ili kufanya kampeni za amani na heshima.

Pia amewahimiza wanasiasa kuuza sera zao kwa wananchi kwa wakati unaofaa, akitaja baadhi ya miradi ya maendeleo aliyotekeleza wakati wa uongozi wake.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment