Highlights

Wakaazi wa  kijiji cha Sukuroi ,Ilaut walalamikia ukosefu wa  maji.

Na Sabalua Moses

Wakaazi wa kijiji cha Sukuroi katika eneo la Illaut, Wadi ya Ngurnit, Kaunti Ndogo ya Korr, wameendelea kulalamikia ukosefu wa maji kufuatia kuharibika kwa kisima pekee kikilicho kuwa kinawahudumia kwa zaidi ya miezi mitano.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, chifu wa Illaut, Philip Lesagaram, amesema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita kumi kutafuta maji baada ya kisima hicho kuharibika.

Lesagaram amesema hali hiyo imeathiri maisha ya wakazi na kutoa wito kwa serikali kuingilia kati haraka ili kurekebisha kisima hicho ili wakazi wapate maji.

Aidha, amesema kuwa wanafunzi katika shule za eneo hilo hulazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kuzingatia masomo yao.

Aidha, kwa upande wake Steve Learbora  mkazi katika  kijiji cha Sukuroi amesema kuwa wamelazimika  kukaa bila maji kwa miezi  mitano suala linalowapelekea kusafiri hadi illaut ili kukata kiu.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment