Wakaazi wa Bori, moyale washutumu viongozi wao kwa kufumbia jicho mahangaiko yao.
Na Samuel Kosgei
Wakaazi wa eneo la Bori eneobunge la Moyale wamefanya maandamano kulalamikia ukosefu wa maji na huduma za matibabu katika eneo hilo.
Wakaazi hao wamelalamikia ukosefu mkubwa wa maji ambayo wanasema kwa muda mrefu wamehangaika kutokana na visima kukauka na kukosekana kwa mvua.
Masuala mengine wanayolalamikia ni ikiwemo huduma duni za matibabu, barabara mbovu na ukosefu wa mtandao wa simu suala wanalosema inazuia kilio chao kusikika.
Wameshutumu viongozi wao wa mashinani na wa jimbo kwa kuwapuuza na kutowatafutia suluhu la matatizo wanayopitia.
Wakaazi hao sasa wanamwomba rais William Ruto kuingilia kati na kuwanusuru kwani viongozi wao wamewapuuza na kufumbia jicho matatizo yao. Wanasema bado wana Imani na serikali kuu kuwa itawapa sikio.



Post Comment