Loading Now

Highlights

Wakaazi mjini Marsabit wakashifu kuenea kwa magenge ya kisiasa nchini

Na Sabalua Moses

Baadhi ya wakaazi mjini Marsabit wamekashifu kuendelea kuibuka kwa magenge ya kisiasa huku uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ukikaribia.

Wakizungumza na Shajara wakaazi hao wameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kukomesha magenge hayo kwa kuwekeza katika kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia nafasi za ajira na miradi ya maendeleo.

Vilevile wamedai kuwa ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umechangia wanasiasa kuwatumia vijana katika kuzua rabsha za kisiasa.

Aidha baadhi yao wamewahimiza vijana kutafuta njia mbadala za kujipatia riziki na kujiepusha na siasa za vurugu zinazotishia amani na mshikamano wa taifa.

Post Comment