Kina mama Laisamis waongoza mapambano dhidi ya mila potofu.
NA Nyabande Orwa
Huku baadhi ya mila na tamaduni zikiendelea kushikiliwa katika eneo bunge la Laisamis, hali imeanza kubadilika kwa kina mama waliopata elimu na kuwezeshwa kiuchumi.
Haya yamebainika katika mkutano uliowaleta pamoja wazee na kina mama kujadili umuhimu wa kujitegemea kiuchumi na kuachana na tamaduni zinazowaathiri vijana.
Katika mkutano huo uliodhaminiwa na shirika la Pastoralist People Initiative PPI, kina mama kutoka makundi mbalimbali wamesema kuwa kupitia uwezeshaji huo wamepiga hatua katika kupambana na mila kama ukeketaji na ndoa za mapema. Wamesema pia kuwa sasa wanahamasisha elimu, na wasichana wanaokimbia ukeketaji au ndoa za mapema wanapewa nafasi ya kurejea shuleni.
Wakati huo huo, wamepongeza wazee kwa kukubali kutoa ardhi kwa ajili ya miradi ya maendeleo itakayosaidia kusomesha watoto na pia kupambana na matumizi ya dawa za kulevya katika eneo la Laisamis.



Post Comment