Highlights

Ngamia walioibwa Wajir Magharibi warejeshwa baada ya kupatikana Laisamis.

NA Nyabande Orwa

Maafisa wa usalama katika eneo bunge la Laisamis wamefanikiwa kurejesha ngamia sita wanaodaiwa kuibiwa kutoka Wajir Magharibi wiki moja iliyopita.

Akithibitisha tukio hilo, Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Laisamis, Kepha Mwaribe, amesema kuwa maafisa wa usalama kwa ushirikiano na wazee wa eneo hilo walifanikiwa kuwapata ngamia hao na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Laisamis.

Mwaribe amekanusha madai kuwa wezi wa mifugo walijaribu kushambulia kituo hicho cha polisi Ijumaa iliyopita, akisema kuwa mchakato wa kuwakabidhi ngamia hao kwa wamiliki wao ulifanyika kwa amani.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa machifu kuhakikisha watoto wote wanaofaa kwenda shule wanarejea masomoni shule zitakapofunguliwa, ili kusaidia kukabiliana na visa vya wizi wa mifugo katika eneo hilo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment