Highlights

Wachezaji 4,950 wasajiliwa kwenye FIFA Connect kuinua kiwango cha soka Marsabit.

NA JB Nateleng

Jumla ya wachezaji 4,950 kutoka Kaunti ya Marsabit wamesajiliwa katika mfumo wa FIFA Connect, hatua inayolenga kuimarisha na kuinua kiwango cha soka katika eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa shirikisho la soka Kenya (FKF) tawi la Marsabit, Godana Roba, amesema usajili huo utasaidia wachezaji kutambulika kimataifa, huku kila mchezaji akipewa namba maalum katika mfumo huo.

Godana pia amesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, shirikisho hilo limefanikiwa kutoa mafunzo kwa marefa na makocha ili kuboresha maendeleo ya soka jimboni.

Aidha, amewahimiza makocha kujitolea zaidi katika kutambua na kukuza vipaji vya vijana, akisisitiza kuwa kuna vipaji vingi vinavyohitaji kulelewa kwa uadilifu.

Pia ameahidi kuwa shirikisho hilo linaendelea na mipango ya kuhakikisha timu zote katika Kaunti ya Marsabit zinashiriki katika ligi ijayo.

Hata hivyo, Godana ametaja ukubwa wa kaunti ya Marsabit pamoja na changamoto za miundombinu kuwa kikwazo katika utekelezaji wa majukumu ya shirikisho hilo. Amesema licha ya changamoto hizo, ushirikiano kati ya viongozi, wachezaji na makocha ni muhimu ili kufanikisha usajili na ushiriki wa ligi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
Loyd Dehart

Hi,

I help businesses turn underperforming websites into growth assets.

With over 15 years of experience in Web Development and SEO, I support companies in increasing visibility, attracting qualified traffic, and converting visitors into customers.

If improving your online performance is a priority this year, I would welcome a brief conversation.

Post Comment