Highlights

Vijana Marsabit watakiwa kufahamu hali yao ya virusi vya ukimwi.

Na Sabalua Moses

Wito umetolewa kwa vijana katika Kaunti ya Marsabit kujitokeza kupima na kujua hali yao ya maambukizi ya virusi vya ukimwi badala ya kutegemea taarifa kutoka mitandaoni kutafuta matibabu.

Kwa mujibu wa muuguzi anayeshughulikia masuala ya ukimwi katika hospitali ya rufaa ya Marsabit, Rose Nyeusi, vijana wengi hutegemea mitandao ya kijamii na programu za akili unde badala ya kutafuta huduma za afya kutoka kwa wataalamu hospitalini.

Aidha, Rose amezihimiza jamii kuachana na mila na desturi zinazowazuia watu kujitokeza kupima na kujua hali zao. Pia ametoa wito wa kukomeshwa kwa unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment